Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi kutoka Jeshi la Wanachi Tanzania akipata maelezo kutoka Taasisi ya mafunzo ya Afya Ifakara iliyoandaa Mfumo wa Kitaifa wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (National eLearning Platform for Health). Mfumo wa Kitaifa wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao ni mfumo uliotekelezwa na Taasisi ya mafunzo ya Afya Ifakara (TTCIH) kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto chini ya ufadhili wa Global fund, mfumo huu unapatikana kupitia tovuti http://elearning.moh.go.tz. Mfumo huu unawezesha wataalam-wanafunzi kujipatia mafunzo ya miongozo mbalimbali ya utoaji huduma za afya, Pia mfumo huu ni stahimilivu wenye uwezo wa kufanya kazi bila kuhusisha mtandao muda wote(Online and Offline Accesible). Kwa watumiaji wa mabaraza ya afya taarifa zao zinachukuliwa moja kwa moja(Integration) kutoka kwenye mabaraza yao walio sajiliwa ambapo taarifa zitumikazo kuingia kwenye mfumo ni sawa na taarifa(barua pepe na nywila) wanazotumia kuingia kwenye mifumo yao (Single login), mfumo huu unafanya kazi kwenye kitarakilishi (Computer) na Simu janja (Smartphone). Tukio hili limefanyika katika Halmashauri ya Ifakara katika mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021