Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzanian Training Centre for International Health, (TTCIH) anawatangazia umma nafasi za kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2024/2025. TTCIH ni taasisi ya mafunzo ya Afya Ifakara iliyosajiliwa na NACTVET kwa namba HAS/003, Chuo kipo Ifakara mjini, Mkoani Morogoro. Chuo kina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja wakufunzi wabobezi katika masomo yote, Hospitali ya kujifunzia, maktaba bora na masomo kwa njia ya kielektroniki yaanieLearning.
Chuo Kinatoa Kozi Zifuatazo
Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) – Miaka Mitatu
Stashahada ya Utabibu ya Mwaka Mmoja (Yaani upgrading from Clinical Assistant to Clinical Officer).
Stashahada ya Ufamasia (Diploma in Pharmaceutical Sciences) – Miaka mitatu
Stashahada ya Optometria (Diploma in Optometry) – Miaka mitatu
Sifa za Mwombaji kwa Kozi ya Stashahada ya Utabibu ya Miaka Mitatu awe :
Amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Chemistry na Physics
Sifa za Mwombaji wa Stashahada ya Utabibu Mwaka Mmoja (Yaani Upgrading From Clinical Assistant to Clinical Officer ) awe :
Amehitimu Astashahada ya Utabibu (Technician Certificate in Clinical Medicine).
Sifa za Mwombaji kwa kozi ya stashahada ya Ufamasia (miaka mitatu) awe :
Amehitimu kidato cha nne kwa ufaulu wa angalau D ya Biology na Chemistry
Sifa za Mwombaji kwa kozi ya stashahada ya Optometria (Miaka mitatu) awe :
Amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Chemistry, Basic Mathematics, English na Physics/Engineering Sciences
Jinsi ya Kujaza Fomu za Maombi
Maombi yote ya kujiunga na Chuo yanatumwa kupitia tovuti ya NACTVET kwenye kiunganishi (QUICK LINK ) kilichoandikwa MAOMBI YA UDAHILI VYUO VYA AFYA 2024,Kwa msaada wa kujaza FOMU MOJA KWA MOJA CHUONI, tafadhali jaza taarifa zako kwenye hii fomu hapa chini kisha bofya “SEND” dawati la usajili litakupigia simu muda wowote kukusaidia kujaza fomu kikamilifu au piga simu namba zifuatazo (+255) 0718365374, 0718 552 164, 0758943044 & 0710527003
KARIBU TTCIH IFAKARA KWA MAFUNZO YENYE KUJENGEA WAHITIMU UWEZO KUTOA TIBA KWA KUTUMIA TAFITI YAANI EVIDENCE BASED MEDICINE