Nafasi za Kujiunga na Chuo kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzanian Training Centre for International Health, (TTCIH) anawatangazia umma nafasi za kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2022/2023. TTCIH ni Taasisi ya mafunzo ya Afya Ifakara iliyosajiliwa na NACTVET kwa namba HAS/003, Chuo kipo Ifakara mjini, Mkoani Morogoro.

  • Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) – Miaka Mitatu
  • Stashahada ya Utabibu ya Mwaka Mmoja (Yaani Upgrading from Clinical Assistant to Clinical Officer).

Sifa za Mwombaji kwa Kozi ya Stashahada ya Utabibu ya Miaka Mitatu awe

  • Awe amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Chemistry na Physics

Sifa za Mwombaji wa Stashahada ya Utabibu Mwaka Mmoja (Yaani Upgrading From Clinical Assistant to Clinical Officer )

  • Awe  amehitimu Astashahada ya Utabibu (Technician Certificate in Clinical Medicine).

Chuo kina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja wakufunzi wabobezi katika masomo yote, Hospitali ya kujifunzia, maktaba bora na masomo kwa njia ya kielektroniki yaani eLearning

 

Maombi yote ya kujiunga na Chuo yanatumwa kupitia tovuti ya NACTVET  kwenye kiunganishi (QUICK LINK ) Kilichoandikwa MAOMBI YA UDAHILI VYUO VYA AFYA 

KARIBU TTCIH IFAKARA KWA MAFUNZO YENYE KUJENGEA WAHITIMU UWEZO KUTOA TIBA KWA KUTUMIA TAFITI YAANI  EVIDENCE BASED MEDICINE

Kwa msaada na maelekezo zaidi piga simu namba(+255) 0758943044 || 0787629707

 

 

 

Share:
Previous Post
Newer Post