Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Ifakara (Tanzanian Training Centre for International Health ) – TTCIH kilichopo mjini Ifakara Mkoani Morogoro anawatangazia umma kwamba sasa Chuo kinapokea maombi ya kujiunga na Chuo kwa mwaka wa masomo 2024/225 kwa kozi zifuatazo;
- Stashahada ya Optometria (Diploma in Optometry) – Miaka Mitatu
- Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) – Miaka Mitatu
- Stashahada ya Ufamasia (Diploma in Pharmaceutical Sciences) – Miaka Mitatu
Sifa za Muombaji kwa Kozi ya Stashahada ya Utabibu (Miaka Mitatu) awe:
- Amehitimu kidato cha nne kwa ufaulu wa angalau D ya Biology, Chemistry na Physics
Sifa za Muombaji kwa Kozi ya Stashahada ya Ufamasia (Miaka Mitatu) awe:
- Amehitimu kidato cha nne kwa ufaulu wa angalau D ya Biology na Chemistry
Sifa za Muombaji kwa Kozi ya Stashahada ya Optometria (Miaka Mitatu) awe:
- Amehitimu kidato cha nne kwa ufaulu wa angalau D ya Biology, Chemistry, Basic Mathematics, English na Physics/Engineering Sciences
TTCIH ni Chuo cha Serikali kilichosajiliwa na NACTEVET kwa namba HAS/003 kinachoendeshwa chini ya Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka inchini Uswiss. Chuo kina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja Wakufunzi waliobobea katika fani za Afya na tafiti, Hospitali ya kujifunzia kwa vitendo, Internet ya uhakika, na kutoa mafunzo kupitia Mfumo wa Mafunzo kwa njia ya Masafa – (National eLearning Platform for Health – www.elearning.moh.go.tz) ambao unasimamiwa na Wizara ya Afya. Kwa kujaza fomu moja kwa moja Chuoni na maelekezo zaidi piga simu namba zifuatazo +255 710 527 003, +255718 552164, +255758 943 044, 0718365374 na tembelea tovuti yetu wwww.ttcih.ac.tz au tutumie barua pepe info@ttcih.ac.tz
“KARIBU TTCIH IFAKARA KWA MAFUNZO YENYE KUJENGEA WAHITIMU UWEZO KUTOA TIBA KWA KUTUMIA TAFITI YAANI EVIDENCE BASED MEDICINE”