TTCIH Imeshiriki Kwenye Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu – Zanzibar

TTCIH tumepata fursa ya kushiriki kwenye Maonesho ya Saba (7) ya Wiki ya Elimu ya Juu yanayoendelea (14 – 20 Julai 2026) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Tumepata heshima ya kutembelewa na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Shaaban Ali Othman – Kaimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Shaaban Ali Othman ameipongeza TTCIH Ifakara kwa kushiriki katika maonesho haya, akibainisha kuwa chuo hiki ni miongoni mwa taasisi chache za mafunzo ya afya ngazi ya Diploma kutoka Mkoa wa Morogoro zilizoshiriki maonesho haya. Ameeleza kuwa ushiriki wa TTCIH ni hatua muhimu ya kuwatambulisha wananchi wa Zanzibar fursa mbalimbali za elimu zinazotolewa na chuo, pamoja na kuwarahisishia waombaji kupata taarifa na kujaza fomu za kujiunga kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Tunakukaribisha kutembelea banda letu ili ujifunze zaidi kuhusu Chuo cha TTCIH Ifakara, kozi mbalimbali tunazotoa, sifa za kujiunga, na huduma nyingine zinazopatikana chuoni.

Aidha, utapata fursa ya kujionea Mfumo wa Mafunzo kwa Njia ya Masafa (National eLearning Platform for Health – NELP) unaopatikana kupitia www.elearning.moh.go.tz, ambao umeasisiwa na TTCIH kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya kupitia Idara ya Mafunzo.

Watoa huduma wetu watakuwa tayari kukuelekeza kuhusu kozi mbalimbali na kukusaidia hatua kwa hatua katika kujaza fomu za kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Chuo Kinatoa Kozi Zifuatazo:

  1. Stashahada ya Ufamasia (Diploma in Pharmaceutical Sciences) – Miaka mitatu
  2. Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) – Miaka mitatu
  3. Stashahada ya Optometria (Diploma in Optometry) – Miaka mitatu

#Kwa msaada na maelekezo zaidi piga simu namba zifuatazo:

0718 365 374 & 0718 552164

“KARIBU TTCIH – IFAKARA KWA MAFUNZO YENYE KUJENGEA WAHITIMU UWEZO WA KUTOA TIBA KWA KUTUMIA TAFITI YAANI EVIDENCE BASED MEDICINE”.

 

Share:
Previous Post