Ziara ya Wataalamu wa Afya kutoka Chuo Kikuu cha ATHENS – Ugiriki

Wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Athens – Ugiriki, wakiongozana na wenyeji wao kutoka Tanzanian Training Centre for International Health (TTCIH) – Ifakara, leo tarehe 25 Agosti 2026, wametembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mheshimiwa Wakili Dastan Kyobya.

Ziara hiyo imelenga kujifunza na kuona kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Wakili Dastan Kyobya amewapongeza wataalamu hao kwa ushirikiano wao na TTCIH, ambao umekuwa na mchango mkubwa katika kuwajengea ujuzi na kuongeza weledi katika taaluma ya afya.

Aidha, Mheshimiwa Kyobya amewasihi kuendelea kuitangaza Wilaya ya Kilombero pamoja na fursa na vivutio vyake vya utalii, ili kuwahamasisha wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani kuitembelea Kilombero na kujionea uzuri na fursa zilizopo.

Share:
Previous Post